MICHEZO

SIMBA YA MWENDOKASI YAENDELEZA UBABE DHIDI YA STAND UNITED

img_4382
Simba SC imevunja rekodi ya Stand United ya kutofungwa kwenye uwanja wao wa nyumbani kwenye msimu huu, baada ya kuichapa kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Shiza Kichuya aliifungia alikwamisha bao pekee kwenye mchezo huo lililoipa Simba pointi tatu dhidi ya Stand United. Kichuya alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penati dakika ya 33 baada ya mshambuliaji Laudit Mavugo kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Awali Stand United walikuwa hawajapoteza mchezo kwenye uwanja wao wa nyumbani, walipoteza mchezo wao wa kwanza kwenye ligi msimu huu waliposafiri kuifuata Tanzania Prisons ambapo walifungwa bao 2-1 kwenye uiwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Ushindi wa leo wa Simba unaifanya iendeleze rekodi yake ya kutopoteza mchezo hadi sasa baada ya kucheza mechi 13, imeshinda mechi 11 na kutoka sare kwenye michezo miwili.
Sasa Simba imefikisha pointi 35 na kuendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 8 baada ya watani zao wa jadi kupoteza mchezo wao dhdi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.
  • Simba imekuwa timu ya kwanza kupata ushindi dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa Kabarage Shinyinga.
  • Stand United wamepoteza mchezo wao wa pili baada ya kuondoka kwa kocha wao mkuu Patrick Liewig aliyeicha timu ikiwa haijapoteza mchezo hata mchezo mmoja. Stand ilifungwa kwa mara ya kwanza na Prisons kwenye uwanja wa Sokoine (Tanzania Prisons 2-1 Stand United na Stand United 0-1 Simba).
  • Kichuya amefikisha mabao 9 katika mechi 13 alizochea kwenye ligi msimu huu amezifunga timu zote za Shinyanga. Alifunga goli moja kwenye ushindi dhidi ya Mwadui (Mwadui 0-3 Simba na Stand United 0-1 Simba.
  • Musa Ndusha amecheza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi msimu huu baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mwinyi Kazimoto.

No comments:

Post a Comment