Wednesday 2 November 2016

SIMBA YA MWENDOKASI YAENDELEZA UBABE DHIDI YA STAND UNITED

img_4382
Simba SC imevunja rekodi ya Stand United ya kutofungwa kwenye uwanja wao wa nyumbani kwenye msimu huu, baada ya kuichapa kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Shiza Kichuya aliifungia alikwamisha bao pekee kwenye mchezo huo lililoipa Simba pointi tatu dhidi ya Stand United. Kichuya alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penati dakika ya 33 baada ya mshambuliaji Laudit Mavugo kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Awali Stand United walikuwa hawajapoteza mchezo kwenye uwanja wao wa nyumbani, walipoteza mchezo wao wa kwanza kwenye ligi msimu huu waliposafiri kuifuata Tanzania Prisons ambapo walifungwa bao 2-1 kwenye uiwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Ushindi wa leo wa Simba unaifanya iendeleze rekodi yake ya kutopoteza mchezo hadi sasa baada ya kucheza mechi 13, imeshinda mechi 11 na kutoka sare kwenye michezo miwili.
Sasa Simba imefikisha pointi 35 na kuendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 8 baada ya watani zao wa jadi kupoteza mchezo wao dhdi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.
  • Simba imekuwa timu ya kwanza kupata ushindi dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa Kabarage Shinyinga.
  • Stand United wamepoteza mchezo wao wa pili baada ya kuondoka kwa kocha wao mkuu Patrick Liewig aliyeicha timu ikiwa haijapoteza mchezo hata mchezo mmoja. Stand ilifungwa kwa mara ya kwanza na Prisons kwenye uwanja wa Sokoine (Tanzania Prisons 2-1 Stand United na Stand United 0-1 Simba).
  • Kichuya amefikisha mabao 9 katika mechi 13 alizochea kwenye ligi msimu huu amezifunga timu zote za Shinyanga. Alifunga goli moja kwenye ushindi dhidi ya Mwadui (Mwadui 0-3 Simba na Stand United 0-1 Simba.
  • Musa Ndusha amecheza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi msimu huu baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mwinyi Kazimoto.

PENDEZA NA BIDHAA ZETU POPOTE ULIPO TUTAKUFIKISHIA KWA BEI NAFUU


Sunday 30 October 2016

Ajali Dar


Basi la Safari Njema likiteketea kwa moto
       
Basi la abiria lililokuwa likitokea Dodoma liitwalo Safari Njema lenye namba za usajiri T 990 AQF limegongana na lori lenye namba ya usajili 534 BYJ eneo la Kimara Stop Over Jijini Dar es Salaam na kusababisha kuwaka kwa magari hayo yote mawili na kupelekea kifo cha abiria mmoja na majeruhi 10.

HESLB yatoa tamko


Image result for Abdul-Razzaq Badru
 Mkurugenzi wa Bodi ya mikopo Elimu ya juu Abdul-Razaq Badru akizungumza na waandishi wa Habari
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB), imetangaza mpango wa kupitia upya na kusitisha mikopo wanafunzi wote inaodai kuwa walipewa mikopo lakini hawakidhi vigezo vipya vya utolewaji wa mikopo hiyo,
Akizungumza na waandishi wa habari  mkurugenzi wa Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu Abdul-Razaq Badru ametaja wanafunzi wanaostahili kupata mikopo kuwa ni yatima, walemavu au wenye wazazi wasiojiweza pamoja na wale wanaosoma masomo ambayo ni miongoni mwa vipaumbele vya taifa.
“Kwa vigezo hivi, muombaji anayesoma fani za sayansi za tiba na afya, ualimu wa Sayansi na Hisabati, uhandisi (Viwanda, Kilimo, Mifugo Mafuta na Gesi) au yatima, mlemavu na mwenye wazazi wenye hali duni au wasiojiweza ndiye anayestahili kupata mkopo.
HESLB tutahakiki upya wanufaikaji wa mikopo waliopo mwaka wa pili, tatu na hata wale wa mwaka wa nne ili kuondoa kila asiye na sifa na kwa wale wa mwaka wa kwanza waliokosa mikopo na wanadhani wanazo sifa wakate rufaa  kuanzia Novemba Mosi,” amesema Badru.
Wakati HESLB ikijiandaa kufanya hivyo, Kilonzo Mringo, Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFMSO) amesema iwapo bodi ya mikopo itafanya hivyo, wanafunzi wengi watashindwa kuendelea na masomo.
“Mpaka sasa IFM wanafunzi wengi wana sifa na wamenyimwa mikopo, wengine wameamua kusitisha masomo yao na wengine wanasoma kwa kuja chuo wiki moja, nyingine wanaenda kutafuta fedha. Hali ni mbaya, wakiamua kupunguza tena idadi ya wanaopata mikopo basi chuo kitabaki kitupu,” amesema Mringo.
Eliudi Kasunzu, Waziri wa Mikopo katika Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) ameiambia MwanaHALISI Online kuwa hawapingi zoezi la uhakiki lakini wanaishangaa HESLB kuhakiki wanaopata mikopo ambao ni wachache na kuacha kuhakiki wengi walionyimwa.
“Hatuoni mantiki ya kutuhakiki tena kwa kuleta dodoso wanafunzi wajaze, fomu za maombi wanazo huko ofisini kwao wakihitaji kuhakiki basi waziangalie na si kutuingiza kwenye usumbufu wa kujaza dodoso wakati hivi karibuni wamefanya uhakiki wa idadi ya wanufaikaji.
“Hata vigezo walivyoweka mwanzo hawazingatii, tuna orodha kubwa ya wanafunzi yatima, walemavu na wanaosoma masomo yanayotajwa kuwa ni vipaumbele vya taifa lakini bado wamenyimwa mkopo halafu wanataka wachache waliopata wawapunguze zaidi,” amesema.
Boniface Emmanuel, Waziri Mkuu wa DARUSO yeye amesema anadhani kitendo cha HESLB kutaka kuhakiki wanafunzi wanaoendelea na masomo ni mbinu ya kuchelewesha kuwapa fedha zao za kujikimu.
“Kama mtu aliomba mkopo mwaka mmoja, miwili au mitatu iliyopita na akaonekana kwa bajeti na uchambuzi wa wakati huo ana vigezo vya kupata mkopo, iweje umuhakiki mwaka huu? Nadhani wanatafuta kisingizio cha kuchelewa kulipa fedha za kujikimu za awamu zijazo kwa kisingizio cha uhakiki,” amesema Boniface.
 Source Mwanahalisi Online..